My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, October 18, 2011

mambo muhimu ya kufanya ili kijana ajikomboe kimaisha sehemu ya 2

UNACHOTENDA
Ukiangalia tabia ya maisha ya mwanadamu utagundua kuwa anafahamu mambo mengi sana, lakini hatendi sawa na ufahamu wake. Naamini hata vijana wanajua njia za kufanikiwa, lakini hawazifuati.

Binafsi kuwafundisha watu kile wanachokifahamu ni sawa na ujinga. Kamwe siwezi kutumia muda wangu kuwaambia vijana ili waendelee wanahitaji kufanya biashara, kuajiriwa, kujiajiri kulima, kwani kufanya hivyo ni kukosa shabaha ya elimu.

Ukitaka kuthibitisha hili zungumza na vijana wanaoishi maisha magumu uone kama hawatakuorodheshea njia zaidi ya 100 za kufanikiwa kimaisha! Kumbe tatizo lao si kujua bali ni kutenda ambako ndiyo njia ya kuelekea kwenye mafanikio.

Wewe kama kijana jaribu kukumbuka ni biashara, mradi, kazi gani uliyokwishaiwaza na mpaka leo hujaanza kuifanya kwa sababu ambazo hazifahamiki? Miongoni mwa watu wenye tatizo hili wapo ambao si tu kwamba wana wazo, wana fedha, nguvu bali wana uwezo wa kufanya mambo yakawezekana, lakini wamejikuta hawafanyi yale wanayoyaweza na hivyo kubaki watumwa wa umasikini wakiamini tu kuwa, ipo siku wataanza na kufanikiwa.

Tatizo kubwa katika mgando huu wa mawazo ni woga wa kushindwa na ugumu wa kuanzisha jambo. Wanasema waswahili ‘MWANZO MGUMU’ hata hivyo haiwi sababu ya wengi kushindwa kufanya mambo kwa kuhofia kukutana na ugumu. Watu wengi waliofanikiwa duniani ni wale ambao walikuwa tayari kuingia katika hatua hii muhimu ya kutenda yale waliyoyawaza na kuyathibitisha kuwa yatasukuma mbele maisha yao.

Wote tunajua mwanzo wa kila kitu ni wazo, lakini mawazo yasiyokuwa na matendo ni upuuzi! Vitu ambavyo vimekuwepo duniani na vitakavyokuwepo baadaye vitatokana na ushirikiano wa hatua hizi mbili yaani KUAMINI NA KUTENDA. Ni wakati wako wa kuamini au kugeuza mawazo yako kuwa vitu halisi.

Umewaza sana kujenga nyumba mbona hujaanza kujenga? Unasubiri nini kuanza biashara uliyoifanyia utafiti na ukagundua kuwa itakuingizia kipato. Nani kakuzuia usipange chumba chako na kuanza maisha yako? Amka na uanze kufanya yote uliyoyawaza!

UNACHOCHAGUA
Katika hali ya kawaida mwanadamu wa kawaida ana mahitaji mengi yanayotoka kwenye vitu vingi pia. Ukihitaji mchumba kwa mfano, itakulazimu hitaji lako likutane na wingi wa wachumba tofauti tofauti. Changamoto utakayokutana nayo wakati utakapokuwa unataka kutenda ulichoamini ni kuchagua.

Tambua kuwa chochote utakachotaka duniani hakiko peke yake, ukienda sokoni kununua nyanya, utakutana na mafungu mengi ya bidhaa hiyo kiasi cha kukufanya utumie akili kuchagua fungu moja au mawili unayohitaji.

Kuwepo na vitu vingi vya kuchagua kama nilivyosema ni moja kati ya tatizo kubwa linalowafanya vijana wengi washindwe kufanikiwa kimaisha kutokana na kutokuwa makini wakati wa kuchagua. Wapo ambao wameshindwa kuendelea kwa sababu tu walichagua wake wabaya, biashara, fani, kazi, kilimo kibaya na mambo mengine.

Inawezekana kabisa pengine hata mambo ambayo yanakuendea kombo leo yametokana na kosa lako la kuchagua. Ushauri wangu ni kwamba kila mtu anayetaka kufanikiwa kimaisha lazima ahakikishe mambo anayoyachagua yawe ni yale aliyoyahakiki kuwa yanafaa.

TUNACHOPATA
Katika hali ya kawaida hakuna mtu anayetafuta kila siku asipate, hili halina ubishi, labda kinachoweza kuwa tofauti ni kiwango cha kupata.

No comments:

Post a Comment

New