My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, October 29, 2011

Dotnata awachana wavaa nusu utupu

Na Mwandishi Wetu
Staa wa filamu, muziki na mjasiriamali Bongo, Husna Posh ‘Dotnata’ (pichani) ameibuka na kuwaponda wasanii hususan wacheza filamu wanaovaa nusu uchi na kuwaambia kwamba kufanya hivyo ni zaidi ya kujidhalilisha.

Dotnata anayekimbiza sokoni na filamu yake ya Chupa Nyeusi aliyowashikirisha wasanii wa Burundi, akichonga na paparazi wetu hivi karibuni katika viunga vya Msasani Beach Club Kinondoni, alisema anawashangaa mastaa wanaopenda kuvaa nguo fupi sana na kukatiza mitaani bila kujali kama wao ni kioo cha jamii.

“Unajua sisi wasanii hasa wanawake tunapaswa kuwa mstari wa mbele kusimamamia maadili kwa sababu ni kioo cha jamii, sasa tunapovaa nguo fupi zinazotuacha nusu uchi na kukatiza mitaani jamii ituelewaje?” alihoji Dotnata.

Msanii huyo aliongeza kuwa thamani ya ustaa ni kujiheshimu na kuvaa nguo za heshima jambo linaloweza kuigwa na jamii kuliko mambo yasiyofaa kama ulevi, uasherati na kutembea nusu uchi.

No comments:

Post a Comment

New