My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, October 27, 2011

VITA KALI YESU Vs FREEMASONS...

Jamii za siri zilizopo kwenye kundi la Dini za Shetani, Freemasons, Illuminati na Skull & Bones zipo kwenye vita nzito na ujio wa Yesu (Isa bin Mariam), shabaha yao ikiwa kuuteka ulimwengu kabla ya kiongozi huyo anayebeba imani za Kikristo na Kiislam hajaja.

Uwazi limeelezwa kuwa Dini za Shetani zipo kwenye mapambano makubwa zikitaka kutimiza dhamira zao za kuifanya dunia iwe inaabudu dini moja na kutumia sarafu moja kabla ya ujio wa Yesu.
Imebainishwa kuwa njama za Dini za Shetani zipo tangu karne tatu zilizopita na mpango wao mwingine ni kuhakikisha dunia inatawaliwa na serikali moja.


Vyanzo mbalimbali vinasema kuwa taarifa kuwa Yesu ameonekana ziliishtua jamii ya Dini za Shetani kwa sababu ni pigo kubwa Yesu kurejea kabla wao hawajatimiza azma yao.

Ripoti za mitandao ya intaneti na nukuu za mtaalamu wa mambo ya jamii hizo za siri, Maalim Hassan Yahya Hussein, zinabainisha kuwa ndani ya Dini za Shetani kuna vita ya wao kwa wao, kila moja ikitaka yenyewe ndiyo itawale dunia.
Maalim Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, hayati Sheikh Yahya Hussein, alisema kuwa Freemasons ndiyo jamii ya siri yenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani, hivyo ni rahisi kufanikiwa kuliko Illuminati na Skull & Bones.

“Angalia kila upande wa dunia, Freemasons wameweka nguvu yao. Tanzania wapo, wamewashika viongozi. Tazama Marekani, hivi sasa ili mtu awe rais ni lazima awe Freemason,” alisema Maalim Hassan ambaye ndiye mrithi wa kazi za marehemu Sheikh Yahya.

rafu yenye namba 666. Hayo mambo yanakuja, ni njama zao. Freemasons ni Dini ya Shetani kwa sababu inaongozwa na Jini Mkuu anayeitwa Lucifer ambaye anapigania kuiteka dunia kwa kuwateka wapenda dini, Wakristo au Waislamu.”
Alisema, kutokana na msimamo wa dini hizo za mashetani, hawawezi kukubali Yesu aje duniani, kwani atafanya mambo yaliyo kinyume na wao.

“Wakristo wanasema Yesu akirudi duniani atalinyakua kanisa (wateule wake), hii ina maana atawapa pigo kubwa, kwani atawafanya washindwe kuitawala dunia. Kwa Waislamu, ujio wa Yesu ni ishara ya kiyama, kwa hiyo ni vita ya kugombea ukubwa.

“Freemasons, Illuminati na Skull & Bones, kila moja inataka ukubwa, inapigania kuitawala dunia. Yesu akirudi pia atafanya Neno la Mungu litawale. Unadhani hiyo siyo vita? Dini za Shetani zimejipanga kikamilifu kutawala dunia kabla Yesu hajarudi.”

Alisema ili kutimiza nia yao hiyo, wamekuwa wakijitahidi kueneza matawi yao karibu kila nchi duniani na kushika maeneo muhimu ya kiuchumi, kijeshi na hata kisiasa, na kugawa waumini hali inayodhihirisha kuwa lengo lao la kuitawala dunia limepamba moto.

Akaongeza kuwa Ijumaa wiki hii atakwenda Arusha na moja ya mambo atakayozungumza na watu wa huko ni hili la Freemasons kwani wamekuwa wakimpigia simu kutaka kujua zaidi.
Wachungaji, maaskofu wazungumza

Baadhi ya wachungaji wa makanisa waliozungumza na gazeti hili kuhusiana na vita hiyo walikiri kwamba ipo.
Mchungaji wa Kanisa la House of Prayer Information, Dar es Salaam, Kaleb Simbe alisema dini hiyo ya kishetani siyo rahisi kuwepo makanisani na hata mali walizonazo waliomo katika dini hiyo wanazipata kwa njia chafu.

Alisema utajiri wa baadhi ya waumini wa dini hiyo unaweza kuwafanya baadhi ya watu kuvutiwa na kujiunga nao lakini nguvu ya Yesu ni kubwa, wanajikuta wakishindwa.
Askofu Chessa Elias wa Kanisa la Victorious Tabata, Dar alisema haamini kama waumini wa dini hiyo wapo makanisani kwa sababu imani zao ni tofauti.

No comments:

Post a Comment

New