My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, October 29, 2011

Ugumu wa maisha usipunguze raha ya mapenzi


MUHALI gani mabibi na mabwana wale wote ambao huwa tupo sambamba katika kuhakikisha hamuikosi safu hii. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu natumaini wote mu wazima wa afya njema, kwa wale walio wagonjwa Muumba awape nafuu ili mpone upesi.

Naam leo najua kina baba mmekaa tayari kujua kwa nini niwaite wavivu, nina maana yangu, ni ukweli ulio dhahili kuwa kina baba wengi kutokana na ugumu wa kazi na mawazo mengi kichwani au ugumu wa maisha ya maana kila kukicha hali inakuwa ni afadhali ya jana.

Mmejikuta muda mwingi hamfikirii masuala ya mapenzi zaidi ya kufikiria baada ya kula leo, ungoje kesho yake itakuwaje.
Hata mkeo akitaka haki yake utampa tu ili mradi, kwako huwa ni karaha na kuona kama usumbufu. Kama ulimzoesha kumliza kilio cha mbwa, anakuwa hakipati tena, basi zinakuwa lawama kila kukicha.

Siku zote ili ufurahie penzi lazima moyo wako uwe umetulia na mawazo yako yaweze kuwaza kile ukifanyacho. Lakini unawaza ugumu wa maisha mkeo naye anataka haki yake asilimia 100.

Lakini ugumu wa maisha upo hata ufanyeje, la muhimu japo hukufanikiwa kupata chochote urudipo nyumbani muone mkeo kama tulizo lako. Usifikiri ni wewe unayeumia bali hata yeye vile vile anaumia kwa kuona unataabika bila mafanikio.

Hivyo basi, unaporudi hujitahidi kumliwaza kwa mapenzi motomoto kwa kuwa starehe ile huilipii, angalau mioyo yenu muipe chakula chake. Usiwe mkosa yote, fedha hukupata na hata mkeo hukumridhisha.

Hata kazi nzito hupoteza hamu ya kufanya mapenzi, kwa mwanamke lazima umjue mwenzio yupo kwenye hali gani, najua umeshikika na wa kukutuliza ni mumeo mpe nafasi angalau apumzike kidogo, kisha ruksa kuurudisha mwili wake kwenye hali ya mapenzi kwa kuuandaa mwili, kwa kumshika zile sehemu zinazoupa mwili msisimko kwa haraka.

Lazima atajisikia hamu ya mapenzi, hapo lazima uwe makini kwa kujua mwenzio pamoja na kumrudisha katika hali ya mapenzi bado mwili wake hautakiwi kazi nzito tena bali unatakiwa kumpa penzi laini ambalo halitamchosha sana na kuuchosha mwili wake zaidi.

Hapa lazima mwanaume awe mbunifu kwa mtindo wa njia ya mkato ambao utawahisha kumfikisha kileleni haraka mwanamke bila kuuchosha sana mwili wako.
Siku zote mwanaume unatakiwa kumsoma mkeo ili kujua njia ipi ya haraka kumfikisha mwenzako au penzi la muda mrefu la kuinjoi unapokuwa na nguvu za kutosha.

Kwa utaratibu huu nina imani malalamiko ndani ya nyumba zetu yatakwisha, mwisho namalizia kwa kusema kuwa ugumu wa maisha usipunguze upendo ndani ya nyumba kwa kumnyima mwenzio haki yake, nawe mwanamke ukimuandaa mwenzio raha zako utazipata.

No comments:

Post a Comment

New