My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, October 29, 2011

lulu amfuata Mwanaume Marekani

Na Imelda Mtema

Mcheza filamu mdogo ambaye hivi karibuni alipenda aitwe ‘mrs Bieber’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ yupo kwenye maandalizi ya kwenda Marekani kwa ajili ya kumfuata mwanamuziki anayetamba kwa sasa nchini humo, Justine Bieber.

Lulu alizungumza hayo kupitia mtandao wa mtangazaji mahiri wa Televisheni ya Clouds ya jijini Dar, Zamaradi Mketema.

Alisema kwamba endapo atakwama katika suala la nauli, atatengeneza kadi kwa ajili ya kuchangisha michango kwa maana kitendo hicho alichoamua ni cha kijasiri sana kwa vile ni nadra binadamu kujitoa ‘mhanga’ kwenda kumtafuta mtu nje ya nchi.

“Mimi lazima nimfuate, hata kama nauli itanishinda nimeshaandaa mpango wa kuchangisha kwa kupitia kadi ambazo nitazitengeneza, kitendo hiki ni cha kijasiri sana, hakuna mtu ambaye aliwahi kufanya,” alisema Lulu.

Staa huyo aliongeza kuwa endapo atafanikiwa kumuona ‘laivu’ mwanamuziki huyo ndipo mchezo mzima utakapoishia na Watanzania waamini kuwa lazima atamleta Bongo kwa sababu anajua akionana naye hawezi kuchomoa.

“Nitakapoonana naye lazima nitamleta hapa nyumbani kuonesha ushindi wangu kwani najua akionana na mimi kamwe hawezi kuchomoa kwangu,” aliweka wazi Lulu kupitia mtandao huo.

No comments:

Post a Comment

New