My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, October 18, 2011

Utandawazi katika vyakula ndiyo unao tuuwa

KATIKA ulimwengu tunaoishi hivi sasa, binadamu tunakabiliwa na adui mkubwa ambaye ni maradhi. Kama hakuna hatua madhubuti zitakazochukuliwa haraka ili kupambana na adui huyu, huenda kizazi cha sasa na kijacho, kitaishi maisha mafupi sana duniani.

Ili tumshinde adui huyu na tufanikiwe kuishi maisha marefu, hatuna budi kuwa na elimu ya kutosha ya kupambana naye. Ili asisumbuliwe na maradhi, binadamu anahitaji siyo tu kula chakula kizuri, bali kilicho bora na kilisho asilia. Lakini kwa bahati mbaya sana, asilimia kubwa ya vyakula tunavyokula hivi sasa siyo bora na vingi siyo asilia.

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kimezaliwa kitu kinaitwa ‘utandawazi’, ambao umeleta mabaliko makubwa mazuri katika maeneo mengine, lakini umeleta madhara katika eneo la vyakula. Vyakula vingi tunavyokula hivi sasa ni ‘fake’, kuanzia maji tunayokunywa hadi nyama tunazokula kila siku.

UHARIBIFU WA VYAKULA
Vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokunywa karibu vyote ni vya kutengeneza. Maji ya chupa ambayo yanatumika kwa wingi mijini ni maji yaliyopitia kiwandani ili kusafishwa na kuua vijidudu vinavyoweza kusababisha magonjwa ya tumbo. Lakini wakati wa mchakato wa kusafisha na kuua vijidudu hivyo, virutubisho pamoja na ladha asilia ya maji nayo hupotea, hivyo kupoteza madini asilia ya maji.

Kama ukibahatika kunywa maji ya kisima yaliyo safi na salama, ladha yake na faida yake mwilini ni tofauti kabisa na maji ya chupa, bila kujali yanatengenzwa kutoka wapi. Kiasilia maji yana virutubisho na madini muhimu katika mwii wa binadamu na yalikikusudiwa tuyanywe bila kuyachemsha wala kuyawekea kemikali zingine za kuuawa wadudu, kama usingekuwepo uchafuzi wa mazingira unaochafua maji hayo.

MAZIWA
Mbali ya maji, kinywaji kingine kinachohimizwa kutumiwa na watu, wakubwa kwa watoto, lakini kimeathirika, ni maziwa. Ni jambo lilio dhahiri kuwa maziwa ni muhimu kwa binadamu na yana virutubisho na madini mengi yenye faida kwa ustawi wa afya ya binadamu. Lakini ili upate faida hizo, ni lazima unywe maziwa asilia.

Maziwa asili ni yale yatokanayo na ng’ombe waliofugwa na kulishwa vyakula vya asili, kama majani na magome ya miti. Kwa kawaida ng’ombe huishi kwa kula nyasi porini au shambani katika mazingira yaliyohuru yanayowawezesha kuota jua na kunyeshewa na mvua. Ng’ombe anayeishi katika mazingira haya, maziwa atakayo yatoa yatakuwa bora na vivyo hivyo nyama yake.

Lakini katika ulimwengu wa utandawazi tulionao, ng’ombe wengi ni wa kufugwa, ambao hulishwa nafaka badala ya nyasi na kupewa madawa ya kuongeza utoaji wa maziwa. Kitendo cha kumlisha ng’ombe nafaka, kama vile pumba na au mahindi, tayari unakuwa umemkosesha virutubisho muhimu anavyovihitaji ili akutolee maziwa yaliyo bora.

Wanasayansi wengi wamelishaligundua hili na wameanza kulipiga vita kwa kusisitiza watu wapende kutumia bidhaa za wanyama waliofugwa na kulishwa vyakula asilia (organic farming). Kwa sababu ladha na faida za bidhaa za wanyama hao, kama vile maziwa na nyama, zina tofauti kubwa kwa afya ya mlaji.

Kwa upande wa vinywaji baridi ambavyo vinatangazwa kama ‘juisi ya matunda’, ni hatari kiafya. Kwani vinywaji vyote vinavyouzwa kama juisi, vimetengenezwa kiwandani kwa kuchangaya rangi na kemikali za ladha mbalimbali. Kwa maana hiyo, havina virutubisho vyovyote na faida yoyote kwa mlaji, zaidi ya kujiweka katika hatari ya kupatwa na maradhi siku zijazo

No comments:

Post a Comment

New