My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, October 18, 2011

Zijue Tabia 10 hatari katika mapenzi

MADA yetu ya unyumba ni nguzo ya mapenzi, ukiwa mchoyo unabomoa, niliifafanua kwa matoleo mawili mfululizo. Bila shaka, utakuwa umetambua jambo la kuzingatia ili uishi kwa amani. Nyongeza ni kuwa kama binadamu na uhusiano wa kimapenzi, heshima ya kweli ni pale ambapo mwenzi wako anakutunzia ‘tamu’ yako kwenye mazingira yoyote yale.

Akiitoa, ni sawa na kuvuliwa nguo! Pale unapopumzika na wengine hutulia hapo hapo! Hii inamaana kuwa hutakiwi kujiuguza uvivu katika suala la mapenzi. Toa huduma inayotakiwa, ikibidi ongeza vionjo kadiri unavyoweza. Kosa kubwa kwa wengi ni kwamba hawachukulii tendo kama ni jukumu la kutekeleza. Yaani ni wajibu! Wanaona ni kitu rahisi ndiyo maana kila siku wanalia.

Unaacha kutekeleza nguzo hiyo ya uhusiano, matokeo yake mwenzi wako kwa kuzidiwa anaona bora aende akapate tulizo nje. Angalia unavyoweza kubomoa uhusiano wako. Anapoonja pembeni, kisaikolojia na hisia zake akizipeleka huko ni hatari zaidi, kwani anaweza kukuona huna faida.

Ipo mifano mingi ya watu waliosahau nyumba zao kwa sababu ya manjonjo ya nje. Mume kumuona mke wake ni kapi, vivyo hivyo, mke kumshusha thamani mwenzi wake. Hayo yote yanaweza kudhibitiwa ikiwa kutakuwa na maridhiano ya kweli baina ya wanandoa. Anahitaji, jihimu kumtekelezea kwa maana hujui ndani yake kuna nini.

Somo lilikuwa poa sana lakini tuachane nalo na kushika hili la leo. Tunazungumzia mapenzi katika sura ya kipekee kwa kuwa yanahitaji thamani ya hali ya juu. Yanaheshimiwa kupita kiasi kwa sababu yenyewe ni sanaa kiranja ambayo kila mtu lazima atayapitia.

Tunapenda na kupendwa, hivyo tupo mapenzini. Ambaye hayumo, basi pengine mambo yake siyo mazuri. Hata hivyo, binadamu hatuko sawa, kila mtu anayo tafsiri yake anayoijua kuhusiana na mapenzi, ndiyo maana hatuachi kuelekezana. Naandika kwa kushauri na kukosoa kwa sababu huu ndiyo wajibu wangu katika safu hii.

Kila mmoja anapoingia katika uhusiano wa kimapenzi, moja kwa moja ndoto zake huwa ni kumfanya mwenzi wake kuwa wa kudumu. Atajiwekea malengo hata yasiyotekelezeka ilimradi airidhishe nafsi yake.

Hujawahi kuona mtu anapata mwenzi leo, kisha akaanza kupiga mahesabu ya kufunga naye ndoa? Ukweli ni kwamba wengi wetu tunapopata penzi jipya, tunakuwa na matarajio mengi. Ni vizuri kuwa na matarajio na kujiwekea malengo ya kuyatimiza, lakini kosa kubwa ni kwamba huwa tunajisahau katikati ya safari.

Tunapenda kudumu na wenzi wetu tunaowapata, lakini ndoto hizo hugeuka za alinacha kama si kitendawili kwa kuwa hatuwezi kujirekebisha au kuficha makucha. Matunda ya hali hiyo ni kuwa na kizazi chenye kujiwekea matarajio ya ‘blah blah’ kila siku.

Pointi ya msingi hapa kama kweli tunataka kuwa na mapenzi ya kudumu ni kujua udhaifu wetu angali bado mapema. Kutambua mambo ambayo ni sumu zinazoweza kuua uhusiano wetu ili tuzichukue kama changamoto, kisha tuzikabili na kushinda.

Hapa chini, nimekuandalia tabia 10 ambazo ni sumu katika mapenzi. Hizi, zinaweza kuubomoa uhusiano wako ndani ya muda mfupi. Muhimu ni kuzijua ili utambue namna ya kuziepuka.

Unaweza kuziepuka kwa sababu siyo za maumbile, bali ni kujiendekeza. Ukiamini hakuna kitakachoshindikana, kwa hiyo nakuasa uongozane na mimi mdogo mdogo ili upate jawabu la kutosha kuhusiana na mada hii.

UVIVU
Hii ni sumu kali, lakini ni rahisi kuiepuka kama utaamua. Asili ya umbile la kila binadamu, ndani yake kuna uvivu. Ni vizuri kutambua kuwa katika vitu ambavyo ni rahisi kumchefua mwenzi wako ni hili la uvivu.

Uvivu unaweza kuwa wa kujishughulisha katika mambo ya nyumbani ama wa utafutaji wa riziki. Lakini baki ukijua kwamba tabia hiyo inakufanya ukalie kuti kavu kwenye uhusiano wako.

Unashindwa kumsaidia mpenzi wako kazi ndogo ndogo, unangaalia nguo chafu haujitumi kuzifua, nyumba haitamaniki, hujiwezi kwa lolote, tabia yako hiyo, inampa mwenzio tiketi ya kukuacha.
Pointi hii, inastahili kupigiwa mstari mwekundu kwetu sisi wanawake

No comments:

Post a Comment

New