My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, July 30, 2012

BARAZA LA VIJANA CHADEMA(BAVICHA) LAWATAKA VIJANA KUSHIRIKI KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA


Wakazi wa Iringa wakiwasikilizaviongozi wa BAVICHA 
katika uwanja wa Mwembetogwa



Umati wa wakazi wa Iringa ukimsikiliza Katibu wa
BAVICHA Deogratias Munishi

Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa akiongea na wananchi wa Iringa katika 
Viwanja vya mwembetogwa leo hii


Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na maendeleo BAVICHA leo limefanya muendelezo wa ziara zake katika uwanja wa Mwembetogwa mkoa wa Iringa.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na idadi kubwa ya vijana kutoka sehemu mbalimbali za maeneo ya Mkoa wa Iringa. Umekuwa kivutio kikubwa kutokana na viongozi wa BAVICHA kutoa sera zinazohusu maendeleo na mustakabali wa nchi.

Akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu wa BAVICHA taifa Deogratias Munishi amewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kutoa maoni kuhusu kuundwa kwa katiba mpya wakati kamati husika ifikapo katika maeneo wanayoishi ili kuweza kuunda katiba iliyo nzuri na yenye kutetea maslahi ya mwananchi wa kawaida.

Munishi ameongeza kuwa haoni umuhimu wa wakuu wa wilaya na mkoa na kuwataka wananchi kujitokeza kutoa maoni yao na kama kutakuwa na ulzima wa kuwepo kwa viongozi hao basi wachaguliwe na wananchi wenyewe ili waweze kuwajibika ipasavyo kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

New