My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, July 2, 2012

Dk. Mtaki: Usagaji ni starehe kama zingine *Asema ikizidishwa inaharibu saikolojia ya mchezaji



Ibrahim Bakari
GUMZO juu ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars kufanya vitendo vya kustareheshana, limetetewa na baadhi ya wataalam kuwa ni tendo linaloweza kufanyika kama lilivyo tendo lingine.

Mjadala ulizuka wiki mbili zilizopita juu ya kufanya vibaya kwa Twiga Stars kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 na Ethiopia katika mechi za kuwania kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika Equatorial Guinea baadaye Novemba.

Mkwasa alisema kuwa kufanya vibaya kwa timu hiyo kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kuendekeza vitendo vya kusagana, lakini akasema kuwa waliokuwa wakifanya 'hayo mambo' (bila kuwataja) walitimuliwa.

Lakini vitendo hivyo vimetajwa kushamiri hasa katika timu zinazojumuisha wanawake ama wasichana wengi kwani kila mmoja anakuwa na tabia na mihemko yake kiasi cha kuwaathiri wengine.

Spoti Mikiki ilifanya mahojiano na Dk. Magreth Mtaki, daktari wa michezo wa siku nyingi kutoka Kurugenzi ya Michezo ambaye anasema kuwa kusagana (lesbianism) ni kama starehe nyingine ambayo watu wa jinsi mbalimbali wanafanya.

Anasema kuwa tatizo linakuja kuwa ni suala linalohusisha wasichana ama kinamama ndiyo maana linaleta mshangao, lakini hakuna tofauti na matendo mengine ama kustareheshana kwa watu wawili.

Dk. Mtaki ambaye pia ni Makamu wa Chama cha Soka ya wanawake Tanzania, TWFA, anasema kuwa kitendo cha kusagana, kwa upande mwingine kina athari kubwa kwenye timu kwani endapo kitafanywa kwa kuzidisha, inamaliza nguvu mchezaji.

"Hata ingekuwa wewe na mke wako, una mechi ya kimataifa ama ligi, halafu ukafanya tendo la ndoa kupitiliza, ni wazi itapunguza uwezo wako uwanjani, basi hata hawa wanaosagana, wakizidisha, lazima uwezo utapungua.

"Kingine ambacho naweza kusema, lakini sasa hii ni kwa mchezaji mwenyewe...hali hii itamfanya hatokuwa na hamu ya mwanaume akiamini kuwa mwanamke mwenzake anakata kiu.

"Lakini pia kingine ambacho naweza kusema kitachangia timu kufanya vibaya ni kwamba, kama itatokea msichana ana mtu wake halafu akafahamu kuwa fulani anamchukulia, ni wazi kunajengeka chuki miongoni mwao.

"Sasa kutokana na kuwa na chuki na 'mwizi' wake, hata kama atakuwa kwenye nafasi ya kufunga, hawezi kumpa pasi utakuta mtu yuko kwenye nafasi ya wazi, lakini hampi pasi, hiyo inachangia sana kukosa ushindi.

"Hata kama ni mimi...mfano, mimi na wewe hatueleweni, unadhani nitakupa pasi uwanjani?...Unadhani nitakusogelea kukuomba pasi, siwezi kwa sababu tayari nina  kinyongo na wewe kwa kuwa umenichukulia mtu wangu, matokeo yake 'bifu' langu na wewe linaigharimu timu," anasema Dk. Mtaki.

Mtaki alilalamikia wahusika ikiwemo meneja wa timu, Furaha Francis kwa kutolitolea taarifa mapema tatizo hilo kwani halileti picha nzuri katika jamii.

Lakini nahodha wa timu hiyo, Sophia Mwasikili anasema kuwa suala hilo halipo kwenye timu yao kwani kusema Twiga Stars wanasagana, ni kuwavunjia heshima katika jamii inayowazunguka.

"Unafikiri leo hii tuingie uwanjani, kila mmoja anatuona wote wasagaji na wasagwaji...mimi nimekuwa nahodha wa timu tangu 2006, lakini sikuwahi kusikia haya mambo ya kusagana, kwa kweli imetuvunjia heshima sana," anasema Mwasikili anayecheza soka Uturuki katika klabu ya Luleburgazgucu.

Mwasikili alisema kuwa hafikirii wala kudhani kama kulikuwa na tatizo hilo na kama walifukuzwa inawezekana alikuwa anafahamu kwa kushuka kiwango

No comments:

Post a Comment

New