My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, July 14, 2012

Benki za Kiislam zinaweza kuwasaidia wakulima?

Kufuatia ushauri wa waziri mkuu Mizengo Kayanza Pinda wa kuziomba bank zipunguze kiwango cha riba kwa wakulima, kuna swali limeulizwa kua vipi bank za kiIslam zinaweza kuwasaidia wakulima? Swali hilo limejibiwa kama ifuatavyo.  Ni kweli kwamba katika gazeti la Mwananchi la tarehe 16/5/2012 kulikuwa na makala iliyonakili ushauri wa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Kayanza Pinda akizishauri bank zitoe mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima. Alizitaja changamoto ambazo zinawakabili wakulima kwa kusema ‘"Wakulima wadogowadogo wanashindwa kupata mikopo ya kutosha kwa sababu benki za biashara zinawatoza riba kubwa na kuhitaji dhamana (collateral) alisema Mh Pinda. Mh Pinda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hotuba  iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Kilimo Vijijini Afrika (Afraca).
 
Tukianzia na tataizo la riba (interest) na ambalo bank za kawaida zinatofautiana na bank za kiIslam, ni dhahiri kua riba ktk mazingira yake yote ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Matatizo ya riba yalishaelezwa na bado yanaendelea kuelezewa, na kuthibitishwa na wataalam wengi wa kiuchumi duniani, kwa mfano hivi karibuni mkuu wa shirika la fedha la kimataifa  International Monetary Fund (IMF) Christine Lagarde  aliishauri serikali ya Uingereza kupunguza  kiwango cha riba mpaka ifikie sifuri, alinukuliwa akisema “BRITAIN should consider cutting the interest rate to ZERO if the economy continues to struggle, the International Monetary Fund believes”).The Sun 23 may 2012.  Maneno ya Miss Lagarde yaliungwa mkono na wanauchumi wengi kwa kesema  “Cutting rates from 0.5 per cent won’t be the solution on its own, but would send out the right signal.”
 
Kwa upande wa bank za kiIslam, tungezishauri zijitokeze kuwafahamisha wananchi na wadau mbali mbali kua ziko njia mbali mbali zinazoweza kutumiwa kuepuka riba, na wakati huo huo kuleta ufanisi katika nyanja mbali mbali za kiuchumi, jamii na kadhalika. Ukweli ni kwamba bank za kiIslam zina uwezo wa kuwasaidia wakulima kwa kutumia mifumo ya uchumi ambayo inakubalika kisheria kama vile murabaha, mudarabah, muzaarah, musaqaat na nyinginezo ambazo zimeelezewa kwa ufasaha kwenye www.ijuebankiyakiislam@blogspot.com.
 
Tukitolea mfano kwa kutumia mfumo wa murabaha, bank inaweza kuwapatia wakulima vifaa na mahitaji mbali mbali   kwa masharti ya kulipa  hapo baadae pamoja na faida. Murabaha maana yake ni bank au mwenye uwezo, kumnunulia asie na uwezo kitu fulani kwa masharti amlipe kwa faida maalum hapo baadae, kwa mfano bank inaweza kuwanunulia wakulima  vifaa mbali mbali vya kilimo kama vile matrector, mbegu na mbolea, kisha ikawauzia  kwa faida maalum  kwa masharti walipe hapo baadae. hapa inaonekana wazi kabisa kua murabaha unaweza kuwasaidia wakulima wakaweza kujikomboa na kujitegemea hapo baadae.
 
Wasi wasi mwengine ni ule unaohusiana na dhamana (collateral) kutoka kwa wakulima kutokana na uhakika kwamba wakulima wengi hawana mali ambazo wanaweza kuzitumia kama dhamana ili bank ziweze kuwapa mikopo. Hilo nalo linaufumbuzi wake, kwa mfano bank za kiislsm inaweza ikatumia kitu kinachojuikana kama‘group-based lending approach capitalising on peer monitoring and guarantee mechanism’ ambayo ni utaratibu wa kufanya biashara kwa vikundi ambayo hiyo inaweza kuwa mbadala wa dhamana kwa mtu mmoja mmoja.

Ushauri kwa serikali ya Tanzania
 
Kwa upande wa serikali, tunapenda kuishauri ibadilishe njia (approach) katika kilimo na wakulima kwa kuweka mipango madhubuti ya mabaliko katika maeneo mengi ya vijijini kwa kujenga miundominu. Ni ukweli usiopingika kua wakazi wengi wa vijijini wanapoteza haki zao za msingi kama vile elimu bora, matibabu ya uhakika, na kadhalika.  Ukiangalia  umuhimu na mchango wa mkulima katika mataifa yanayoendelea  utakuta kwamba wakazi hawa wanatakiwa wapatiwe mahitaji muhimu kama vile barabara safi, vituo vya elimu, afya na miondombinu mengine.  Kwa kua wakazi wengi wa vijijini ni wakulima, serikali  pia inatakiwa iweke mipango madhubuti ya kuinua kilimo  kwa kuwapatia wakazi hawa wataalam,ujuzi na mahitaji mengine.
 
Pamoja na mambo mengine hotuba yake Mh waziri mkuu  iliziasa bank kuwafikia wananchi huko vijijini, hili ni suala muhimu kwani mabank mengi yamejikita sana mijini na kuwasahau  kwa kiasi  kikubwa wakazi wa vijijini. Wataalamu  wengi wa kiuchumi wanadai kwamba suala la faida kwa mabank ndio sababu ya mabank haya kutokupeleka huduma vijijini,  suala hili limesababisha wakazi wengi wa vijijini kukosa huduma za kibank mpaka waende mijini kitu ambacho kinawagharimu sana. Kwa upande mwengine uchunguzi wa mambo unaonyesha kua wakazi wengi wa vijijini hawana bank accounts, kitu ambacho kimesababisha ugumu sana kwa wakazi hao kuaminika kupata hata hiyo mikopo yenye riba nafuu. Kwa haya machache tunadhani yatasaidia lakin kama kutakua na swali lolote basi usisite kuwasiliana nasi.
 
Kuna ndugu yetu ameuliza swali lifuatalo
 
Asilimia 95 ya wafanyabiashara wa kiIslam hapa TZ wanakopa pesa za riba kutokana na kutokuwepo na taasisi za fedha za kiIslam kuwakopesha, nini hukmu yao ktk nchi hizi ambazo bank za kiIslam hazipo.

Limejibiwa kama ifuatavvyo

Riba ktk mazingira yote imekatazwa ktk sheria ya kiIslam kwa aina zake zote ikiwemo kukopa ambako kuna riba(Quran 03:130; Deuteronomy 23:19 ; Bible, Matthew 05:17). Sio hivyo tu, Mwenye ezzi Mungu ametangaza vita kwa wale wote watakaofanya matendo ambayo riba itahusika kwa njia moja au nyingine. Rudia blog www.ijuebankyakiisam.blogspot.com  kwa maelezo zaidi kuhusu madhara ya riba ktk sehemu ya maswali na majibu kuna article kwa anuani ‘contemporary world without interest’.

Kuhusu kutokuwepo kwa taasisi za fedha za kukopesha bila riba Tanzania, uhakika ni kwamba bank za kiIslam zimeanza kuenea kwa kasi Tanzania ikiwemo Amana bank ambayo ni full Islamic bank na nyingine kama vile NBC ambazo zina Islamic window. Inawezekana kwamba huduma kama za mikopo ya pesa bado hazipo, kama hiyo ndio kesi, basi riba  ktk mikopo itabaki kua ni haramu lakin kuna huduma nyingine ktk hizo bank za kiIslam ambazo ni halali na mteja anaweza akatumia huduma hizo badala ya mkopo wa riba. Kwa mfano anaweza kufanya kitu kinachojulikana kama murabaha, mudarabah, musharaka na nyinginezo ambazo zimeelezewa kwa ufasaha kwenye blog iliyotajwa hapo juu.

Kitu kingine cha kuzingatia ni kwamba mtu kufanya biashara kama hiyo ambayo atahitaji  kuchukua mkopo wa riba, sio kitu cha lazima ambacho asipofanya hivyo atapoteza maisha, kwahiyo, sio ktk dharura zilizoruhusiwa kisheria ya kiIslam ambazo mtu anaweza kufanya jambo la haramu. Ambalo linashauriwa kwa  bank za kiIslam ni kujitahidi kuhakikisha kua huduma hizo zinapatikana hata kama ni ktk wakati wa baadae, kwa kua mahitaji ya huduma hizo yanazidi kuongezeka. Mpaka bank za kiIslam zitakapoanza kutoa huduma hizo mikopo hiyo ya riba itabaki kua ni haram ktk sheria ya kiIslam. Nadhani kwa haya machache yanajibu swali lako na kama utahitaji maelezo zaid basi usisite kutuandikia.
 
Shukran. 
 

No comments:

Post a Comment

New