My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, July 19, 2012

HIVI NDIVYO SHUGHULI ZA UOKOAJI VILIVYOENDELEA KWA ABIRIA WA AJALI YA MELI


 
Baadhi ya miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Seagull.
Baadhi ya wasafiri waliookolewa katika ajali hiyo.
(Picha kwa hisani ya http://zanzibaryetu.wordpress.com/)
MIILI 25 ya watu walifariki katika ajali ya meli ya Seagull iliyozama jana imeokolewa kutoka majini. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar ilizama eneo la Chumbe jirani na Zanzizar. Watu 145 walionusurika katika ajali hiyo wameokolewa wakati watu 120 wakiwa bado hawajapatikana mpaka mwisho wa zoezi la uokoaji lililofungwa jana jioni baada ya giza kuingia. Seagull ilikuwa na abiria 250, watoto 31 na wafanyakazi 9 ikiwa ni jumla ya watu 290. Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni dhoruba kali iliyotokea baharini wakati chombo hicho kikiwa safarini. Zoezi la uokoaji litaendelea leo.

HIVI NDIVYO SHUGHULI ZA UOKOAJI VILIVYOENDELEA
 KWA ABIRIA WA AJALI YA MELI

Mwokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo
Waokoaji wakiokoa moja ya maiti. wakiwa katika boti ya Kilimanjaro.
Majeruhi wakiwa katika mgongo wa boti hiyo wakisubiri kuokolewa.
Baadhi ya Abiria wakiwa katika moja ya chombo cha kuokolea wakielea baharini wakisubiri kuokolewa.
Boti ya KMKM ikiwa katika zoezi la kuokowa majeruhi.

Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko 
katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.  

Daktari akitowa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama ikiktokea Dar-es-Salaam kuelekea Zanzibar









Majeruhi wa ajali ya Meli wakiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakipata huduma baada ya kuokolewa.
Majeruhi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja




Picha ziadi maafa ya meli

Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika meli 
iliyozama hawa ni baadhi ya waliosalimika






Abiria waliookolewa kutoka katika meli iliozama ya 
Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar


Abiria aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama



Abiria aliyookoka katika Meli iliozama ya Star Gate akifarijiwa 
na Jamaa zake Baada ya kuteremka katika Meli iliowaokoa 
hapo Bandarini

HUKu kukiwa bado na tarifa zenye utata juu ya idadi kamili ya waliokufa katika 


ajali ya meli huko Zanzibar ,mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini 
(SUMATRA) imesema, meli iliyozama leo, katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa 
na abiria 248 wakiwemo watoto 31.
Taarifa ya mamlaka hiyo hiyo imesema, meli hiyo, Mv Skagit iliondoka katika Bandari ya
Dar es Salaam leo saa sita mchana, ikiwa na mabaharia tisa.
Kwa mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport, imasajiliwa
na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba, Cheti cha Ubora kimeanza
 tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23 Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa
imeruhusiwa kubeba abiria wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo.
“SUMATRA kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa meli ya 
MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ilikuwa inazama
katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita 
za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar” imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Sumatra, baada ya kupata taarifa hizo, kituo cha MRCC kilitoa taarifa kwa 
vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya usafiri wa majini vilivyokuwa karibu na 
 eneo la tukio.“ Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kwa msaada wa vyombo 
vifuatavyo: Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, 
Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy” imesema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

New