My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, July 1, 2012

VODACOM YATOA TUNZO ZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA‏




Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick Sumaye akimsisitiza jambo Bw.Martin Sanya mara baada ya kumkabidhi tunzo pamoja na kitita cha shilingi Mil 3.8 ya mwamuzi bora wa ligi kuu ya Vodacom 2011/2012, Anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw. Kelvin Twisa.

Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye katikati akishuhudia Mh.Mbunge wa Tabora mjini ambae ni Mwenyekiti wa Simba Sports Club Elden Rage akipongezwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw.Kelvin Twisa mara baada ya kupokea tunzo ya golikipa bora kwa niaba ya Juma Kaseja,wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom.


Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye akiongea wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom.
Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim (kushoto) na Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick Sumaye ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye akimpongeza Msemaji msaidizi wa Azam FC Jaffer Iddi Maganga alipoenda kupokea tunzo ya vijana kwa niaba ya Rashid Mandawa wa Coastal Union wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom,iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika Hoteli ya Dobble Tree, anaeshuhudia kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Bw.Kelvin Twisa.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye katikati akishuhudia Mwenyekiti wa Azam FC Mohamed Said akipongezwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw.Kelvin Twisa mara baada ya kupokea tunzo ya mfungaji bora na timu ya nidhamu na kocha bora kwa niaba ya klabu yake wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom, iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble Tree jijini Dar e Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na tano na laki tano Katibu wa Yanga Bw.Selestini Msigwa wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom, iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble Tree jijini Dar e Salaam,anaeshudia katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twisa.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye kushoto akishuhudia Mwenyekiti wa Azam FC Mohamed Said akipongezwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw.Kelvin Twisa mara baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni ishirini na mbili kwa kuibuka washindi wa pili katika msimu 2011/2012 wa ligi kuu ya Vodacom wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom,iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble Tree jijini Dar e Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye kushoto akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni hamsini Mh.Mbunge wa Tabora mjini ambae ni Mwenyekiti wa Simba Sports Club wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom,katikati ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twisa.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye akipiga picha ya ukumbusho na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom.Iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble Tree Jijini Dar e Salaam.
MWANDISHI WETU
WAZIRI Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ameeleza kusikitishwa kwake na kupoteza umaarufu wa soka la Tanzania kwa sasa ukilinganisha na miaka ya 1970.
Sumaye alisema hayo juzi katika hoteli ya Double Tree By Hilton ya jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwatunuku washindi mbalimbali waliofanya vema kwenye ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/2012.
Alisema hali hiyo inatokana na timu vilabu nguli vya Simba na Yanga kubweteka kwa moja kuifunga nyenzake na kujiona zimefika peponi kitu ambacho si dalili nzuri katika maendeleo ya soka.
“Simba kuifunga Yanga au Yanga kuifunga Simba si kigezo kizuri cha kujiona ni timu nzuri, timu inatakiwa iangalie ushindani kimataifa …ndiyo maana hata wakipangiwa timu kutoka Misri, Ivory Coast n.k mnaingiwa na hofu kubwa,”alisema.
“zamani vilabu vya nje vilikuwa vikipangwa na timu za Tanzania zinatetemeka lakini sisi sasa…kama tunataka kurudi katika heshima yetu ya zamani tujipange kimataifa, “aliongeza Sumaye.
Aidha, Sumaye alisikitishwa na migogoro katika vilabu na kusema inachangia pia kudidimiza soka hivyo amewataka viongozi kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano sambamba na kuvihudumia ipasavyo vilabu vyao.
Sumaye ambaye ni mpenzi mkubwa wa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba, alitumia fursa hiyo kuwaasa mashabiki na wanachama wa timu za Simba na Yanga kuzomeana uwanja pindi moja ya timu inapokuwa uwanjani.
“Muwe wapinzani katika michezo lakini si uhasama, lazima tuwe na urafiki baina yetu na kuonyesha uzalendo zaidi kwa Simba kuishangilia Yanga ikicheza na timu ya nje au Yanga kuishangili Simba ikicheza na timu ya nje,”aliongeza.
Sumaye pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza washindi wote na kuwataka kutovimbishwa vichwa na zawadi hizo badala yake wazitumie kama kichocheo cha kujibiidiisha zaidi.
Awali Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alisema kampuni yake imetoa zaidi ya shilingi milioni 113 kama zawadi za washindi hao na hivyo kufanya mwaka huu zwadi kuongezeka tofauti na mwaka jana zilikuwa shilingi milioni 90.8.
“Tunajivunia kuwa wadhamini wa ligi kuu bara ambapo vipaji vingi vimeonekana na viwango vya kuvutia pia katika mechi zote na ndio maana hii leo tupo katika kutoa zawadi kwa washindi,”alisema.
Katika halfa hiyo, ilitambulishwa tuzo mpya inayohusisha wachezaji vijana waliofanya vema kwenye timu hizo ambapo waliotwaa ni pamoja na Rashid Mandawa (Coastal Union), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting) na Frank Damayo aliyekuwa anaichezea JKT Ruvu na sasa amesajiliwa Yanga ambapo kila mmoja alizawadiwa shilingi milioni moja.
Azam Fc ilifanikiwa kuongoza kwa kutwaa tuzo tano ikiwemo ile ya nafasi ya pili iliyowapatia sh.mil.22, timu yenye nidhamu (mil.7.8), kocha bora-Stewart Hall (mil.3.8), mfungaji bora- John Bocco (mil.3.9) na mchezaji bora- Aggrey Morris (mil.3.3).
Aidha mabingwa Simba walitwaa mil.50, huku kipa wake Juma Kaseja alitwaa tuzo ya kipa bora na kuzawadiwa Mil.3.3, wakati Yanga ilizawadiwa mil.15 kwa kushika nafasi ya tatu na Martin Sanya alitwaa tuzo ya mwamuzi bora na kuzawadiwa mil.3.8.
Ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/2012 ilianza kutimua vumbi Agosti 20,2011 na kumalizikia Mei 6, 2012 na kuvishirikisha vilabu 14 vikiwemo Simba, Yanga, Azam Fc, African Lyon, Kagera Sugar, Mtibwa Sugara, Toto Africans, Moro United, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Coastal Union, Polisi Dodoma na Oljoro JKT.



Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kushoto akiwa na Meneja Masoko wa Vodacom Kevin Twisa 'Kifaa'


Katikati ni Sumaye, kulia Twisa na kuhsoto Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) na mmiliki wa kituo cha Redio cha Voice Of Tabora

Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura kulia

Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala kushoto na rafiki zake

Twisa akihutubia

Mwenyekiki wa Simba, Rage kulia, Mwenyekiti wa Azam, Mzee Mohamed Said katikati na Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa  

Waziri Mkuu wa zamani, kipenzi cha Watanzania, Sumaye

Msaidizi wa Sumaye, Chombo kulia akizungumza na bosi wake

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kulia, katikati Twisa wakiwa na Sumaye

Wadau, Dina Ismail kushoto na Mohamed Mharizo

Warembo wa Vodacom

Maswahiba wa miaka nenda, rudi, Grace Hoka, Mhariri wa BINGWA na Dina Ismail, wa dinaismail.blogspot.com ambaye pia ni Mwandashi wa Habari za Michezo Mwandamizi wa gazeti la Tanzania Daima

Twisa kulia na Sumaye 

Rage na Sumaye wakiteta

Sumaye

Sumaye

Sumaye

Sumaye

BIN ZUBEIRY

Mzee Said kulia, Mwesigwa na Jaffar Iddi, Msemaji wa Azam 

Vimwana wa Vodacom na mataji, tuzo mbalimbali walizokabidhiwa washindi

Refa bora, Martine Sanya kulia akipokea tuzo yake kutoka kwa Mh Sumaye. Kushoto ni Twisa 

Rage amkimpokelea tuzo Kaseja

Mzee Said akipokea tuzo

Mwesigwa akipokea hundi ya Yanga

Mzee Said akipokea tuzo ya Azam FC

Rage akipokea hundi ya Simba SC

Angetile akipongezana na Mh Sumaye

Wadau wa Yanga, katika picha ya pamoja na Mh Sumaye

Wadau wa Simba SC katika picha ya pamoja na Mh Sumaye

Angetile kulia na kushoto Wambura katika picha ya pamoja na Sumaye
Frank damayo

Mlimbwende

Damayo akipokea tuzo yake

Damayo akichukua msosi

Mh Mbunge na kiungo wa zamani wa Simba SC, Rage 'akifakamia' 
JUMA Kaseja, kipa wa Simba SC usiku huu ameibuka kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kujinyakulia kitita cha Sh. Milioni 3.3 kutoka kwa wadhamini Vodacom.
Katika hafla ya kukabidhi tuzo za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom zilizofanyika kwenye hoteli ya Double Tree By Hilton, Masaki, Dar es Salaam, beki wa Azam FC, Aggrey Morris alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi Kuu.
Aidha, Azam FC washindi wa pili wa Ligi Kuu walitwaa pia tuzo za timu yenye nidhamu, wakati kocha waom, Stewart Hall kutoka Uingereza, aliibuka kocha bora, mshambuliaji wake John Bocco ‘Adebayor’ aliibuka mfungaji bora.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah pia alitambulisha tuzo maalum kwa wachezaji chipukizi waliopandishwa kutoka timu za vijana na kufanya vizuri katika timu za wakubwa.
Katika tuzo hizo, kiungo mpya wa Yanga, Frank Damayo sambamba na Rashid Mandawa wa Coastal Union na Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting, kila mmoja alitwaa Sh. Milioni 1.
Katika hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mwamuzi Martin Sanya alishinda tuzo ya refa bora, wakati bingwa Simba alizawadiwa Milioni 50, mshindi wa pili Azam Milioni 22 na Yanga aliyekuwa wa tatu Milioni 15.5.

No comments:

Post a Comment

New