My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, July 14, 2012

Tanzania yapanga kuongeza mara mbili matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanawake kufikia 2015

Rais Jakaya Kikwete alitangaza mpango wa serikali wa kuongeza matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake hadi asilimia 60 kufikia mwaka 2015. Matumizi ya vidonge vya uzazi nchini yalipanda kutoka asilimia 5 mwaka 1989 hadi asilimia 27.4 ya sasa. "Hadi sasa matumizi ni ya kiwango cha chini, lakini tumekusudia kufanya vyema zaidi miaka ijayo," Kikwete aliuambia Mkutano wa Kimataifa wa Uzazi wa Mpango uliofanyika jijini London Julai 11 mwaka huu.

Rais Kikwete aliahidi kwamba ndani ya miaka mitatu ijayo, serikali itajaribu kuongeza mara mbili kiwango cha sasa na kufikia wanawake milioni 4.2 kwa gharama zinazokisiwa kuwa dola milioni 88.2 (shilingi bilioni 138). Serikali pia inapanga kuongeza huduma za wajazito na uzazi kusaidia kuufanya ujauzito kuwa salama zaidi kwa wanawake wa Kitanzania. "Serikali ina bajeti ya uzazi wa mpango kwa vidonge (vya uzazi wa mpango)," alisema. "Inafaidika pia kupitia michango ya mfuko wa washirika wa sekta ya afya, Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Australia."

Kikwete alisema ukosefu wa fedha za kutosha na dhana potofu za jamii dhidi ya uzazi wa mpango, kidini na kitamaduni, ni mambo yanayorudisha nyuma dhamira ya uzazi wa mpango. Mkutano huo wa siku moja wa London ulifadhiliwa na serikali ya Uingereza na Wakfu wa Bill na Melinda Gates kwa msaada wa Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

New