My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, July 2, 2012

Wanamichezo 10 matajiri duniani

PAMOJA na kwamba yuko jela baada ya kushtakiwa na mpenzi wake kuwa hapeleki matumizi, bondia Floyd Mayweather amekuwa mmoja wa wanamichezo matajiri pengine kuliko hata wanasoka mashuhuri.

Kwa kupanda ulingoni pekee, na ushindi wake mara mbili, bondia huyo wa Marekni amekusanya Dola85m na kumpiku Tiger Woods aliyedumu kwa miaka 11 katika chati za wanamichezo matajiri.

Ni ngumu kuamini kuwa bondia huyo anayetumikia kifungo cha siku 90 jela ya Las Vegas baada ya kukwaruzana na mpezi wake wa zamani, na wakati huo alikuwa apambane na Miguel Cotto mwezi uliopita.

Raundi zote 12 za mapambano yake yaliyofanyika Las Vegas, yamemwezesha kuvuna  Dola45m.

Mwingine anayemfuatia ni Manny Pacquiao ambaye katika alimpiga Ricky Hatton na kuzoa Dola23m.

Miongoni mwa wanamichezo 100 waliotajwa kwa utajiri yumo Maria Sharapova, ambaye anashikilia nafasi ya 20, na Li Na, 81 huku David Beckham akishika nafasi ya nane.

Mahendra Singh Dhoni  ni mcheza kriketi mwenye miaka 31 ambaye utajiri wake unafikia Dola26.5m ambazo ni zaidi ya Dola2m za Wayne Rooney.

1. Floyd Mayweather
Bondia (Dola85m)

2. Manny Pacquiao
Bondia (Dola62m)

3. Tiger Woods
Gofu (Dola59.4m)

4. LeBron James
Kikapu (Dola53m)

5. Roger Federer
Tenisi (Dola52.7m)

6. Kobe Bryant
Kikapu (Dola52.3m)

7. Phil Mickelson
Gofu (Dola47.8m)

8. David Beckham
Soka (Dola46m)

9. Cristiano Ronaldo
Soka (Dola42.5m)

10. Peyton Manning
American Football (Dola42.4m)

No comments:

Post a Comment

New