My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, July 18, 2012

SENSA YA WATU NA MAKAZI

SENSA YA WATU NA MAKAZI NI MUHIMU KATIKA MIPANGO
YA MAENDELEO - “Jiandae Kuhesabiwa 26 Agosti 2012”


Historia ya Sensa Tanzania.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603.

Tanzania:Matokeo ya Sensa ya Watu 1967-2002 na Makadirio kati ya mwaka 2003-2025
Mwaka Idadi Mwaka Idadi
1967 12,313,469
2006 38,250,927
1978 17,512,610
2009 41,915,880
1988 23,095,885
2010 43,187,823
2002 34,443,603
2012 45,798,475
2003 34,859,582
2015 49,861,768
2004 35,944,015
2020 57,102,896
2005 37,083,346
2025 65,337,918


Maelezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Sensa ya Majaribio ya Watu na Makazi ya Mwaka 2011.

Sensa ya majaribio ya watu na makazi imefanyika nchini Tanzania katika kaya 5,000. Sensa hiyo imefanyika kwenye maeneo 44 ya kuhesabia watu katika mikoa 11.  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maelezo kwa wananchi kuhusu Sensa ya Majaribio ya watu na makazi ya mwaka 2011.
 
Maswali yaulizwayo mara kwa mara (Frequently Asked Questions)
Sensa ya Watu na Makazi ni nini?
Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kupata na kurekodi habari kuhusu watu na makazi yao.
Bonyeza hapa kupata maswali na majibu zaidi.

No comments:

Post a Comment

New