My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, July 8, 2012

Hotuba ya bwana harusi wetu

Hotuba ya bwana harusi wetu

MC: Na sasa tupate maneno machache kutoka kwa bwana Harusi
BWANAHARUSI: Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu. Pili nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ili kufanikisha harusi hii. Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii. Naishukuru kamati yangu ya harusi kwa kuwezesha kukusanya fedha zilizofanikisha harusi hii, nimshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana. Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na vyakula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, na vijana kwa kuja na pombe za halali na haramu mradi harusi hii ni furaha tupu. MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo aksante sanaaaaa
 
 
 

Mpaka chupi imekonda

Binti alifariki kwa ukimwi. Nyanya yake akawa anakusanya nguo zake ndipo alipokumbana na G String ya marehemu   
BIBI: Sasa nimeamini ugonjwa huu mbaya, umekondesha mpaka chupi
 
 

Mi sina bahati kama mke wangu

Walevi watatu walikutana baa;
Mlevi 1: Hii baa nzuri lakini sio kama ya mtaani kwetu. Pale kwetu kuna baa ya Kimaro ukinunua chupa mbili , Kimaro mwenyewe anakunulia moja nyingine
MLEVI 2: Mtaani kwetu kuna baa ya Gano, hapo ukinunua moja na Gano anakunulia ya pili
 
MLEVI 3: Mtaani kwetu ndio kiboko, kuna baa ya Mzee Komba ukifika akikuchagua, anakununulia bia mpaka ulewe kisha anakupeleka kwenye gesti yake anakupa mtu wa kulala nae
MLEVI 1: Hapo kiboko, we umeshawahi kuchaguliwa?
MLEVI 3: Bado mi sina bahati sana, lakini mke wangu kisha chaguliwa mara 2 wiki hii peke yake.
 
 
 

 
 
 

Aise ufunguo sio wenyewe


Jamaa alikuwa na safari ya miezi kadhaa, kwa wivu wake akamtengenezea mke wake chupi ya chuma. Siku alipokuwa anaondoka akamuita rafiki yake mpenzi;
JAMAA: Aise wewe ndiye rafiki yangu mpenzi mi nasafiri, nimemtengenezea mke wangu chupi ya chuma yenye kufuli, ili wahuni wasije wakamshawishi kunisaliti, sasa naona ufunguo naweza kuupoteza hivyo naomba wewe ukae nao mpaka nirudi.
RAFIKI: Nashukuru kwa imani kubwa uliyonayo juu yangu rafiki, nitakutunzia vema mali zako.......... Mume akaelekea kwenye kituo cha basi, kabla hajafika rafiki yake akamuwahi huku akipumua kwa shida na kutokwa jasho baada ya mbio ndefu.
RAFIKI: Aise samahani, inaonekana umekosea umeniachia funguo sio
 
 
 
 

Nyani na mjusi walikuwa kijiweni wanavuta bangi......

Siku moja Nyani alikuwa kakaa kijiweni anavuta bangi. Mjusi akaja akampa 'Hi', akaomjoin na kuomba puff, nyani akamuonya kuwa ile bangi kali ni kipisi cha kutoka Makete. Mjusi akapokea wakaanza kuvuta kwa raha zao. Mjusi akawa hoi kwa stimu akamwambia nyani,'Nasikia koo limekauka ngoja niende mtoni nikanywe maji'. Mjusi kufika mtoni kwa kuwa alikuwa na stimu nyingi akatumbukia mtoni. Mamba aliyekuwa pembeni akamwona akawahi kumuokoa na kumtoa nje ya maji. Mamba akamuuliza mjusi imekuwaje kutumbukia mtoni kizembe vile, mjusi akajibu, 'Nilikuwa na nyani tunavuta bangi nikasikia kiu cha ajabu nikajikuta kwenye maji' mamba akasema, 'Hebu twende kwa huyo nyani'. Wakamkuta nyani ndo anamalizia kile kipisi hata macho tabu kufungua. Mamba akamuita, 'Oya'. nyani akafungua macho alipomuona mamba akashtuka sana,'Mshikaji umekunywa maji debe ngapi umerudi mkubwa hivyo?
 
 

Vituko vya kweli vya wavuta bangi

Katika maisha yangu nimekwisha sikia vituko vingi kuhusu bangi. Nikikumbuka siku ya kwanza nimemuona rafiki yangu akivuta bangi(1968), jina lake ni Iddi sitataja majina mengine ameshakuwa mtu mzima sasa ninauhakika anawajukuu wengi tu. Alikuja mahala ambapo tulikuwa tunafanya mazoezi ya muziki maana naye alikuwa mpiga gitaa mzuri, akatoa bangi kwenye kibox cha njiti za kibiriti akasokota akavuta, wote tukimkodolea macho na kusubiri apagawe, hakuna cha ajabu alichofanya ila tu nakumbuka alikuwa anarudia rudia na kudai sisi sote ni samaki. Mpaka leo nikikutana nae huwa namtania, 'samaki'.  Rafiki yangu mwingine ambaye ana wadhifa mkubwa serikalini aliwahi kunambia kuwa kuna siku alivuta bangi akahisi shati lake lina siafu, ilibidi alitoe na kulitupa pembeni huku akipiga kelele 'siafu siafu'. Kuna Mzee mwingine Richard, ambaye kwa sasa mawasiliano yetu yamekuwa ni kupitia FB maana miaka mingi hatujaonana, aliwahi kuwa kituko shuleni baada ya kuvuta bangi wakati wa mapumziko ya saa 4, enzi hizo akiwa form 2, yeye alihisi mbingu zinateremka na kuja kumbana, kwa hiyo nae akazidi kutembea huku akiwa ameinama macho yake juu, akiangalia mbingu ambazo kwake zilikuwa zinateremka na kukaribia kumbana, watu wote tukimuangalia na kumshangaa. Sitasahau nilivyocheka kituko cha rafiki yangu marehemu aliyekuwa mwanamuziki muimbaji, ambaye alinambia yeye na rafiki zake mara nyingi walikuwa wanazungumza kuwa kuna wauza bangi huchanganya bangi na kinyesi cha binadamu ili iwe kali zaidi. Sasa siku moja wenzie walipompa kipisi cha bangi, kilianza kumletea hisa za kufa kufa hivyo akahisi 'wamemchanganyia'. Kadri muda ukivyozidi ndivyo alivyozidi kujisikia vibaya, ikalazimu akimbilie kwa baba yake huku akilia,'Baba baba wamenichanganyia'
 
kuna kali ya ukweli ya muuza vinyago(kaajiriwa)..yeye alikuwa anauza vinyago vya kawaida vya mpingo..sasa siku moja akavuta bangi kwa mara ya kwanza tena asubuhi kabla ya kwenda kazini...ila sasa bosi wake jana yake usiku alileta vinyago kutoka Congo(vya kizamani)ambavyo mara nyingi hutoa harufu mbaya sana(sijui kwanini)..sasa jamaa asubuhi akiwa "high"(kwamara ya kwanza) kafungua duka, kasikia harufu mbaya sana, basi akampigia bosi wake;
Jamaa;bosi huku hali ni mbaya sana
Bosi; kwani kuna tatizo gani?
Jamaa:hawa wanyama wote wamekunya humu dukani yani kunanuka kimba balaa njoo mwenyewe uzoe mavi mimi kazi yako basi...  

Wamama natoa onyo, punguzeni ufisadi


Ufisadi unatajwa sana katika mali kama ardhi, na pesa. Utasikia watu wanalalamika ohh Mwenyekiti anahodhi eneo kubwa sana la ardhi peke yake wakati wengine hawana eneo, au ohh jamaa anahodhi akaunti kubwa ya vijisenti wakati wananchi wengine wakiwa hawana hata hela ya kula. Kuna ufisadi ambao uko wazi ila watu wanaukwepa kuupiga vita.
Sensa ya mara ya mwisho hapa nchini,  ilionyesha wazi kuna uhaba mkubwa wa wanaume hapa nchini, sasa unakuta wamama wanahodhi mwanaume na kukataa katakata kushirikiana katika matumizi  kwa ushirikiano na wamama wenzie, huu ni ufisadi wa hali ya juu. Acheni uchoyo, tumieni bidhaa hii adimu kwa ushirikiano, amani na upendo. Nawasilisha hoja
 
 From J. F. Kitime
 

No comments:

Post a Comment

New