My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, July 5, 2012

HONGERA MADAKTARI MUHIMBILI KWA KUMTII RAIS KIKWETE ,HUDUMAZAENDELEA KUIMARIKA MUHIMBILI

  



katika kile kinachoonyesha ni utii kwa Rais Jakaya Kikwete na huruma ya madaktari kwa wagonjwa walikokuwa wakiathirika na mgomo wao huo jana madaktari hao wameendelea kufanya kazi kama kawaida hali inayoonyesha ni uti na inastahili pongezi nyingi kwa madaktari hao kwa kuwa na roho ya huruma .
jana huduma za tiba katika Hospitali yaTaifa Muhimbili zimeendelea kuimarika katika maeneo mengi. Taarifa kutokaKurugenzi ya Tiba (idara ya tiba, idara ya magonjwa ya dharura, idara yawagonjwa wa nje, idara ya magonjwa ya afya ya akili, na idara ya watoto) naKurugenzi ya Upasuaji (idara ya upasuaji, idara ya magonjwa ya wanawake, idaraya meno, idara ya magojwa ya masikio, pua na koo, idara ya macho, na idara yanusu kaputi) imeonyesha kuimarika kwa huduma kwa kiwango kikubwa ukilinganishana hali ilivyokuwa siku chache zilizopita.
ifuatayo ni thathimini iliyofanyikakuanzia asubuhi saa 2:00 hadi saa 11 jioni leo tarehe 4 Julaiy, 2012.
Kurugenzi ya Tiba
Idara ya Tiba: (Internal Medicine)
Madaktari walioko katika mafunzo kwavitendo (Interns) 11wamefika kazini na kufanya kazi. Registrar’s wotewamefanya kazi, Madaktari Bingwa wote wamefanya kazi. Service ward roundszimefanyika pamoja na kliniki ya HIV imefanyika.
Idara ya Magonjwa ya Dharura:(Emergency Medicine)
Madaktari waliokuwepo ni DaktariBingwa mmoja, Registrars wawili na pamoja na Interns wawili.
Idara ya Wagonjwa ya Nje (Cold OPD)
Registrars wote walikuja kazini nawawili wana ruhusa maalum. Wagonjwa wote waliofika walionwa.
Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili(Psychiatry and Mental Health)
Madaktari Bingwa wote walikuwepokazini isipokuwa mmoja ambaye yuko masomoni. Kliniki zote zimefanyika, wagonjwawote waliolazwa wodini wameonwa
Idara ya Watoto: (Pediatrics and ChildHealth)
Madaktari Bingwa wote wamekuja kaznina kufanya kazi. Interns watatu nao walikuja na kufanya kazi.
Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU)
Huduma kwa wagonjwa wote waliolazwachumba cha wagojwa mahututi wameonwa na wanaendelea kuhudumiwa chini yauangalizi wa karibu..
Kurugenzi ya Upasuaji
Upasuaji leo umefanyika na kunaongezeko kubwa la madaktari lililojitokeza leo kwa ajili ya kufanya upasuajikatika vyumba vya upasuaji. Orodha ya wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji keshoAlhamisi Julai 4, 2012 imeandaliwa na wagonjwa wote wamefanyiwa taratibu zotekwa ajili ya upasuaji ikiwemo kushauriwa na kukubali kufanyiwa upasuaji, kupimwaviwango au wingi wa damu kama inatosha mgonjwa kufanyiwa upasuaji pamoja nataratibu nyingine za tiba. Hata hivyo, wagonjwa bado ni wachache wanaokujakliniki na waliolazwa wodini.
Idara ya Upasuaji: (General Surgery)
Idara ya Upasuaji wagonjwa walionwa naMadaktari bingwa tu, hapakuwa na Interns wala Residents. Kliniki zotezilizopangwa kufanyika leo zimefanyika hususani kliniki ya masikio, pua na koo(ENT), magonjwa ya wanawake, macho (ophthalmology), matumbo (gastroentology),njia ya haja ndogo kwa wanaume (urology), ngozi (skin), ART, magonjwa ya moyo(cardiovascular), meno, plastic surgery pamoja na pediatric surgery. Aidhakliniki zote kwa ajili ya wafanyakazi na wagonjwa wa kulipia (private) zotezimefanyika
Idara ya Magonjwa ya Wanawake: (Obstetricsand Gynaecology)
Wagonjwa wote waliolazwa wameonwa naMadaktari Bingwa kwa kushirikiana na Interns wachache waliokuwepo.
Idara ya Meno: (Dental Surgery)
Madaktari waliokuwa zamu walipitaround na waliona wagonjwa wote waliolazwa.
Idara ya Masikio, Pua na Koo:(Otorhinolaryngology)
Makaktari Bingwa walipita wodini kuonawagonjwa waliolazwa na kufanya upasuaji kwa wagonjwa wawili.
Idara ya Nusu Kaputi: (Anaesthesia)
Madaktari Bingwa na wasaidizi waowalikuwepo na kuendelea na kazi kama kawaida.
Idara ya Macho: (Ophthalmology)
Madaktari Bingwa waliona wagonjwa wotewaliolazwa wodini, waliendelea, kliniki na kufanya upasuaji.
Vyumba vya upasuaji: (Theatre)
Urology: Walikuwa na orodha ya upasuaji na walifanya upasuaji wa mtu mmoja.
Pediatric Surgery: Hawakuwa na orodha ya upasuaji kwa siku ya leo
Plastic Surgery: Hawakuwa na orodha ya upasuaji.
Otorhinolaryngology (ENT) Walikuwa na orodha, walifanya upasuaji kwa wagonjwa wawili.
Macho: Wamefanya zote zilizotakiwa
Kurugenzi ya Tiba Shirikishi(Clinical Support Services)
Madaktari wa Radiolojia wote nanewalikuwepo kazini na wamefnya kazi. Hata hivyo eneo hili halikuwa katika mgomo.Upande wa Maabara: huduma zote ziliendelea kutolewa. Pia eneo hili halikuwakatika mgomo.
Idara ya Pharmacy yenye iliendeleakufanya kazi na pia haikuwa katika mgomo. Idara hii pia ina Interns30 na kati yao watatu wako likizo mmoja yuko likizo ya uzazi waliobaki 27 wotewalikuwa kazini na kuchapa kazi.
Idara hii ina Wafamasia 12 ambapo 10kati yao walikuwepo, na wawili wana likizo maalumu. Pharmacy zote zimefunguliwana kufanya kazi. Eneo hili pia halikuwa kwenye mgomo.
Kurugenzi ya Uuguzi na Ubora(Nursing Services and Quality)
Wauguzi wote wanaotakiwa kuwepo kaziniwapo na wanaendelea na kazi. ha
Tathimini ya jumla:
Huduma zimeendelea kuimarika. Wagonjwani wachache. Madaktari wengi wamerudi kazini na wanachapa kazi.
.Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 4, 2012

No comments:

Post a Comment

New