My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, April 11, 2012

Hatimae leo Lulu afikishwa mahakamani Polisi watoa kauli

Mwigizaji wa movie za kitanzania ELIZABETH MICHAEL maarufu kama Lulu mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Tabata, leo asubuhi alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yanayomkabili kuhusu mauaji ya msanii mwenzake wa filamu STEVEN KANUMBA.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.
Wakili alidai kwamba upelelezi haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena tarehe 23 april mwaka huu.
Mshtakiwa alipelekwa mahakamani kwa siri akiwa kwenye gari lenye namba za usajiri T848BNV aina ya Isuzu ambayo pia ilikuwa na number nyingine za usajiri PT 2365 kwenye vioo.
Kwa mujibu wa blog ya Sophiakessy, Mshtakiwa alisindikizwa na askari wawili wa kike na mmoja wa kiume ambapo mstakiwa alikuwa amevalia dira lenye rangi ya njano na mtandio wa pink na ndala nyekundu.
Akiamplfy na millardayo.com Kamanda wa polisi Kinondoni Charles Kenyela amethibitisha hilo kwa kusema hivi ninavyozungumza yuko SEGEREA akisubiri kuanza hatua ya mchakato wa kisheria, imeonekana kwamba iko sababu ya kumfikisha Mahakamani kwa hiyo ametengenezewa mashitaka ya mauaji ambapo kazi yetu imekamilika na sasa atakua kwenye mikono ya jeshi la Magereza ndio wenye dhamana ya kumlinda”
Kuhusu taarifa kwamba sasa hivi Lulu haruhusiwi kuonekana na yeyote hata mama yake kudaiwa kunyimwa nafasi ya kumpa chakula, Kamanda Kenyela amesema “taratibu za magereza kuhusu chakula wanao utaratibu wao na sheria zao na nisingependa kuliingilia kwa sababu hatuwezi kumsemea Lulu, sasa hivi ni mshitakiwa na kitu alichokiandika kama ushahidi hakitakiwi kutolewa hadharani kitakua kinatumika mahakamani kwa hiyo kinachonong’onwa au kuandikwa labda ni speculation za watu, statement yake ni siri na haijawahi kutolewa hadharani hata siku moja”

No comments:

Post a Comment

New