My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, April 9, 2012

UPDATES za Ajali ya Ndege ya ATC huko Kigoma Leo Asubuhi (9/04/2012

hili ni Bawa lililovunjika wakati ikianguka la upande wa kulia






Abiria 35 na wafanyakazi wanne wa ndege ya shirika la Ndege Tanzania (ATC) wamenusurika
katika ajali ya ndege (pichani juu) iliyotokea asubuhi ya leo majira ya 4.15 katika
uwanja wa ndege wa Kigoma.

kaimu kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya amesema aina ya ndege ni
Dash 8 Q 300 air Tanzania flight No. TC 119 iliyokuwa na abiria thelathini na tano
na staff wanne

Alisema ndege hiyo ilikuwa inatoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora kabla
ya kupata ajali baada ya kuteleza na kuangukia ubavu wa kulia kutokana na tope jingi
lililokuwepo katika njia ya kurukia ya uwanja huo.

Abiria na wafanyakazi wote waliokuwemo waliweza kutoka katika ndege salama muda mchache
baada ya jaribio lake la kupaa angani liliposhindikana.

baadhi ya abiria waliohojiwa baada ya ajali wamewasifia sana rubani Emmanuel Mshana
na msaidizi wake Mbwali masesa kwa kujitahidi kuidhibiti kiuweledi ndege hiyo na
kuokoa maisha ya watu.

Uchunguzi wa awali unaonyesha bawa la kulia pamoja na injini ya propela ya upande
huo vimeharibika vibaya.


huyu ni mmoja wa Abiria aliyenusurika kwenye ajali hiyo akihojiwa.




kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma SSP Kihenya Kihenya (kulia)
akiwa eneo la tukio na maafisa wengine.

No comments:

Post a Comment

New