My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, April 13, 2012

KIJANA WA MIAKA 13 AWAOKOA WENZAKE

Mtoto Jeremy akiliendesha basi baada ya dreva kuzimia.




JEREMY WUITSCHICK, kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 13 kutoka Jimbo la Washington, Marekani, amepongezwa kwa kuweza kushika usukani wa basi la shule na kuliongoza baada ya dreva wake kuzimia Jumatatu wiki hii.
Kijana huyo alionekana kwenye video za kunasa matukio (CCTV) akiliendesha basi hilo hadi sehemu salama na kisha kuzima injini yake baada ya kuanza kwenda mrama katika viunga vya mji wa Tacoma.
Wakati akilisimamisha basi hilo, ofisa mmoja wa shule ambaye alikuwa anashuhudia tukio hilo, alifika na kutoa huduma ya kumrudishia fahamu dreva huyo. Vilevile, polisi walifika hapo na kuwaondoa wanafunzi 12 waliokuwa katika basi hilo.
“Kila mtu alikuwa ananiuliza nilifanyaje,” alisema Jeremy akijibu maswali, na kuongeza: “Nilichofanya ni kuliendesha basi na kulisimamisha pembeni, jambo ambalo kila mtu alilifurahia.”
Dreva alikimbizwa hospitali, hakutajwa jina lake na hali yake haijulikani hadi sasa.
Hivi sasa, Jeremy anataka kuchukua kozi ya huduma ya kutoa huduma ya kushitua mioyo ya watu waliozimia ili waendelee kupumua (cardiopulmonary resuscitation).

No comments:

Post a Comment

New