My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, April 12, 2012

MAMLAKA YA HALI YA HALI YA HEWA

MAMLAKA YA HALI YA HALI YA HEWA NA UBABAISHAJI WA TSUNAMI , DR. AGNES KIJAZI WAOMBE RADHI WATANZANIA KWA KUONGOPA

Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dr.Agnes Kijazi
Kwa utendaji kazi huu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini kuna haja ya mkurugenzi wake Dkt Agnes Kijazi kuwajibishwa kwa kulidanganya Taifa na kuwafanya watanzania kuishi kwa hofu zaidi kwa utendaji wa mkurugenzi huyo .
Mkurugenzi Dr.Kijazi na watendaji wenzake wameonyesha kushindwa kazi hiyo kutokana na kuendelea kuliweka taifa katika hofu kubwa .

Leo mida ya saa 8 za mchana vyombo mbali mbali vya habari zimekuwa vikiripoti juu ya kutokea kwa mawimbi ya Tsunami mida ya saa 12 za jioni ila usiku huu nimetazama habari ya Chanel Tena mida ya saa 1 mkurugenzi huyo ametangaza kuwa Tsunami hakuna tena na wananchi waendelee na shughuli zao.

Japo dakika kama Ishirini hivi kituo cha TBC kilikatisha matangazo kutoka bungeni Dodoma na kuhojiana na mkurugenzi huyo na mkuu wa mkoa wa D,Salaam ambao waliwataka wananchi kuwa makini na Tsunami sasa Dr,Kijazi anataka kulieleza taifa kuwa anafanya kazi kama mganga wa kienyeji ,hapana nasema iwapo Tsunami haitatokea leo ni vema Dr Kijazi kujiuzulu tumechoka kuendelea kusikia ubabaishaji huu.

TAARIFA YA AWALI HII HAPA CHINI.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imetoa tahadhari kwa wananchi waliopo karibu na maeneo ya Bahari ya Hindi kuchukua tahadhari kwa kuondoka katika maeneo hayo kutokana na kuwepo kwa Mawimbi makubwa ya Tsunami kuanzia saa Kumi na Mbili Jioni.

Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dokta AGNES KIJAZI ameiambia Uhuru FM Mawimbi hayo ya Tsunami yanatokea nchini Indonesia katika Jimbo la Ashi kuanzia leo majira ya Jioni.

Maeneo yaliyotolewa tahadhari hiyo ni pamoja na maeneo yaliyopo katika Ukanda wa Pwani, Mtwara, Lindi, Zanzibar pamoja na Wavuvi wanaofanya shughuli zao katika Bahari ya Hindi.

Kuhusu Mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa Dokta KIJAZI amesema hazina uhusiano wowote na Mawimbi hayo ya Tsunami.

No comments:

Post a Comment

New