My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, April 11, 2012

Waziri wa Michezo alichokisema kwenye Msiba wa Steven Kanumba

Msibani Leaders,

Katika Maziko ya mwigizaji STEVEN KANUMBA, Waziri wa habari Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi alitoa kauli kuhusu Marehemu Kanumba na Waigizaji wa movie za kitanzania kwa ujumla.

Nchimbi amesema “tulikua tumefika hatua nzuri sana, tulipenda kijana wetu Kanumba ashuhudie matunda hayo, katika nchi nyingine zinazotazama vizuri taratibu hizi mtu akiigiza filamu moja anatoka kimaisha…. habaki masikini, Tanzania bado hatujafika hapo kwa sababu Kanumba aliigiza filamu zaidi ya arobaini lakini hakufika hapo, hakuweza kuwa tajiri”

Ameamlfy zaidi kwamba “tumepiga hatua, nataka kuwahakikishia watanzania kwamba mawaziri Waziri wa Fedha, wa Viwanda na biashara pamoja na mimi tumekubaliana kimsingi kwamba kuibiwa kazi za wasanii mwaka huu itakua mwisho, tunataka wasanii wetu wanufaike na jasho lao ambapo katika hotuba ya bajeti July mwaka huu mambo ya serikali kuinua kazi za wasanii yatawekwa waziwazi”

Kwa kumalizia Nchimbi alisema “natoa wito kwa wasanii wa filamu Nchini, nilianzisha mazungumzo nao kuhusu umuhimu wa kupatana na wote walikua tayari kupatana, naomba muungane, mpendane, mshirikiane, migogoro kati yenu iishe ili tunapoanza mwezi wa saba, mwezi ambao ni ukombozi kwa wasanii wa Tanzania tuanze ukiwa na tija”

No comments:

Post a Comment

New