My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, April 10, 2012

LULU: NAOMBA MNISAMEHE

Elizabeth Michael ‘Lulu’.


Marehemu Steven Charles Kanumba "The Great" wakati wa uhai wake.

Na Shakoor Jongo
MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam, amesema anaomba msamaha kwa Watanzania kutokana na kifo cha muigizaji maarufu nchini, Steven Kanumba aliyefariki Aprili 7, mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wetu aliyekwenda kumjulia hali huku akiwa mikononi mwa dola, Lulu alisema anaomba msamaha kutokana na kuhusishwa na kifo cha Kanumba, kilichotokea baada ya hali ya kutoelewana kutokea baina yao.
Akisimulia mkasa huo wa kuhuzunisha, Lulu alisema: “Kwanza mpaka sasa siamini kama Kanumba amefariki dunia, nikithibitisha kuwa amekufa na kuzikwa, nitajiua kwa kunywa sumu.”
Aliongeza kuwa kinachomsikitisha zaidi ni kwamba tangu Kwaresma ianze, alikuwa hajawahi kwenda kwa Kanumba, siku aliyokwenda ndipo tukio hilo la kusikitisha lilipotokea.
Lulu anaisaidia polisi kwa kuwa inadaiwa kuwa kabla ya kifo cha msanii huyo nguli, walizozana na marehemu nyumbani kwake, Vatican Sinza baada ya kupokea simu ambayo Kanumba alidhani amepigiwa na mwanaume mwingine.

No comments:

Post a Comment

New