My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, April 27, 2012

JK aongoza watanzania sherehe za Muungano



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza maadhimisho ya mika 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipowasili katika uwanja wa Uhuru kuongoza sherehe za Muungano zilizofanyika  jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo.
Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki, wakionyesha manjonjo ya michezo na maumbo mbalimbali wakati wa sherehe hizo

No comments:

Post a Comment

New