My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, April 16, 2012

RAIS KIKWETE AWASILI BRAZIL KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TANO


Mke wa Rais Mama Salma kikwete akipokea shada la maua mara baada ya yeye na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwasili Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo. Kulia kwake ni Rais Kikwete na nyuma kulia ni Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman na mwenye miwani ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mh Francis Malambugi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Bw Raymond Mbilinyi, baada ya kuwasili Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mwandishi Mwandamizi wa Habari Leo na Daily News, Bw Joseph Lugendo, alipokuwa analakiwa baada ya kuwasilii Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo. Kulia ni Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Msaidizi Mwandamizi wa Rais (Diplomasia) Balozi Liberata Mulamula baada ya mkutano wa maandalizi ya ziara yake ya siku tano nchini Brazil Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo. Katikati ni Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman.
PICHA, HABARI: IKULU
------
Rais Jakaya Mrisho kikwete amewasili Brazil Jumapili Aprili 15, 2012 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tano.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dilma Varna Rousseff wa Brazil na Rais Mstasafu wa nchi hiyo Mheshimiwa Inacio da Silva Lula na viongozi waandamizi wa nchi hiyo.
Katika ziara hiyo, Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi zinazoshiriki katika Mpango wa Ubia wa Uwazi Serikalini (Open Government Partnership-OGP) utakaofanyika mjini Brasilia chini ya Uenyekiti wa Rais Rousseff na kuhudhuriwa na wajumbe wapatao mia nne (400) kutoka serikalini, Asasi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi pamoja na Mashirika ya Kimataifa.
Ubia wa Uwazi Serikalini au kwa kifupi OGP, ni mpango uliozinduliwa Septemba 2011 mjini New York, Marekani kwa lengo la kuwapa wananchi nafasi ya kushiriki katika kuamua mambo yanayowahusu, kupitia vyama visivyo vya Kiserikali na vya Kijamii.
Ubia huu unashirikisha kwa usawa wawakilishi wa serikali kwa upande mmoja na wawakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali za Kijamii kwa upande mwingine. Nchi ya Brazil kwa kushirikiana na Marekani imekuwa mstari wa mbele katika kusukuma ubia huu.
Rais Kikwete anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 17 Aprili, asubuhi mara tu baada ya hotuba ya ufunguzi itakayotolewa na Mwenyekiti wa mkutano huo Rais Dilma Rousseff wa Brazil, ambapo ataelezea maendeleo iliyofikia katika kuandaa mpango kazi wa kutekeleza ahadi ya kuongeza uwazi kama ilivyokubaliwa katika kikao kilichofanyika Disemba 2011. Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 20 Aprili, 2012.

No comments:

Post a Comment

New