My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, April 10, 2012

Safari ya Mwisho ya Marehemu Steven Charles Kanumba kwenye Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar mchana huu

Safari ya Mwisho ya Marehemu Steven Charles Kanumba kwenye Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar mchana huu

Kamanda Kova akiweka mambo sawa mara baada ya watu kuzidi kusogea sehemu ya kaburi,na kufanya shughuli ya mazishi kusimama kwa muda..
Waziri Nchimbi akijadiliana jambo na baadhi ya wanakati ya mazishi ya marehemu Kanumba mchana huu.
Mh. Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo pia yupo makaburini hapa kuhakikisha shughuli inakwenda sawa.
Waombolezaji.
ulinzi upo na ulikuwa ukijitahidi kwa kila hali kuwadhibiti watu wasisogee sehemu lilipo kaburi la Kanumba.
kwakeli watu ni wengi sana makaburini hapa na kuna wengine ambao wanaanguka kwa kukosa hewa,ila vijana wa red cross wako makini katika hilo.
Wanahabari nao wanapata picha kwa shida sana maana watu ni wengi kupita kiasi makaburini hapa.
Waombolezaji wengine wakiwasili makaburini hapo.
Mama wa Marehemi Steven Kanumba akiwasili Makaburini hapa akiwa ameambatana na Dada Asha Baraka.
Muda mfupi uliopita kuna watu ambao walikuwa juu ya mti namna hii na tawi la mti limekatika na kuna baadhi ya watu wameumia na kukimbizwa hospitali.na Kamanda Kova ametoa amri kwa watu wote walio juu ya Miti washuke mara moja maana wanaweza kupata madhara makubwa zaidi.

No comments:

Post a Comment

New